Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
jogoonews.over-blog.com

news,sport,footbal,video,picture,comedy,ubbuyu,vichekesho,habari,taaria,breaking news

Madhara ya kutokuka chakula milo yote

Watu wengi, hasa wanawake wanaamini kuwa ili upunguze uzito wa mwili kwa urahisi na kwa haraka zaidi ama kubakia katika umbo zuri na lenye mvuto ni lazima kuruka mlo mmojawapo kati ya Chai ya asubuhi, chakula cha mchana, au chakula cha jioni.

Kwa mujibu wa myaalamu wa lishe kutoka ‘Family Nutrionist Uganda’, Jamiru Mpiima anasema kuwa kuacha kula mlo mmoja kati ya tuliyoizoea kwa siku ni hatari sana kwa afya.

Dada mmoja wa mapokezi katika kampuni moja ya ujenzi, Faith Drusilla baada ya kujifungua hakuamini umbo lake alipokuwa akijiangalia kwenye kioo. Alijiona kuwa ni mnene sana na umbo lake la kirembo lilipotea. Unene ule ulimtisha kiasi akaamua kuacha kula baadhi ya milo kwa siku ili arudie katika umbo lake la awali. Lakini hakujua kuwa hali ile itamfanya kukosa maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto wake.

Kama Drusilla, wanawake wengi wamekuwa wakiacha kula baadhi ya milo kwa siku ili tu wapungue uzito.

Mpima anasema kuwa kuacha kula huwa na madhara kama vile kukaukiwa na maji mwilini, ambayo hutokea pale mwili unapoishiwa na maji kutokana na mtu kutokunywa maji ya kutosha. Anesema kuwa, watu wanaporuka baadhi ya milo, husahau kunywa maji au vinywaji vingine  na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu hupelekea kukauka kwa maji mwilini.

Kwa kuongezea kunakuwa pia na baadhi ya vitamini na madini  ambayo hukosekana. Kwa ujumla unapoacha kula baadhi ya milo huupelekea mwili kukosa nguvu. Pia hupunguza nguvu ya kinga ya mwili jambo ambalo huweza kusababisha magonjwa.

Mpima amewaonya wanawake kuwa kuacha kula baadhi ya milo kunaweza kuleta mkanganyiko katika mzunguko wao wa hedhi kutokana na kuharibika kwa usawa wa homoni. Mzunguko wa hedhi unaweza kuwahi ama kuchelewa au kutotokea kabisa. hii ni kwa sababu baadhi ya virutubishi vinapohitajika ili kukamilisha mzunguko hukosekana.

Kuvimbiwa pia huweza kusababishwa na mtu kuacha baadhi ya milo ili apunguze uzito. Hii huchangiwa na mzunguko kidogo wa chakula katika mmeng’enyo jambo ambalo hupelekea choo kuwa kigumu na kusababisha maumivu wakati wa kujisaidia na hata tumbo kuuma.

Chanzo: The Citizen

Watu wengi, hasa wanawake wanaamini kuwa ili upunguze uzito wa mwili kwa urahisi na kwa haraka zaidi ama kubakia katika umbo zuri na lenye mvuto ni lazima kuruka mlo mmojawapo kati ya Chai ya asubuhi, chakula cha mchana, au chakula cha jioni. Kwa mujibu wa myaalamu wa lishe kutoka ‘Family Nutrionist Uganda’, Jamiru Mpiima anasema kuwa kuacha kula mlo mmoja kati ya tuliyoizoea kwa siku ni hatari sana kwa afya. Dada mmoja wa mapokezi katika kampuni moja ya ujenzi, Faith Drusilla baada ya kujifungua hakuamini umbo lake alipokuwa akijiangalia kwenye kioo. Alijiona kuwa ni mnene sana na umbo lake la kirembo lilipotea. Unene ule ulimtisha kiasi akaamua kuacha kula baadhi ya milo kwa siku ili arudie katika umbo lake la awali. Lakini hakujua kuwa hali ile itamfanya kukosa maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto wake. Kama Drusilla, wanawake wengi wamekuwa wakiacha kula baadhi ya milo kwa siku ili tu wapungue uzito. Mpima anasema kuwa kuacha kula huwa na madhara kama vile kukaukiwa na maji mwilini, ambayo hutokea pale mwili unapoishiwa na maji kutokana na mtu kutokunywa maji ya kutosha. Anesema kuwa, watu wanaporuka baadhi ya milo, husahau kunywa maji au vinywaji vingine  na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu hupelekea kukauka kwa maji mwilini. Kwa kuongezea kunakuwa pia na baadhi ya vitamini na madini  ambayo hukosekana. Kwa ujumla unapoacha kula baadhi ya milo huupelekea mwili kukosa nguvu. Pia hupunguza nguvu ya kinga ya mwili jambo ambalo huweza kusababisha magonjwa. Mpima amewaonya wanawake kuwa kuacha kula baadhi ya milo kunaweza kuleta mkanganyiko katika mzunguko wao wa hedhi kutokana na kuharibika kwa usawa wa homoni. Mzunguko wa hedhi unaweza kuwahi ama kuchelewa au kutotokea kabisa. hii ni kwa sababu baadhi ya virutubishi vinapohitajika ili kukamilisha mzunguko hukosekana. Kuvimbiwa pia huweza kusababishwa na mtu kuacha baadhi ya milo ili apunguze uzito. Hii huchangiwa na mzunguko kidogo wa chakula katika mmeng’enyo jambo ambalo hupelekea choo kuwa kigumu na kusababisha maumivu wakati wa kujisaidia na hata tumbo kuuma. Chanzo: The Citizen

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post