Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
jogoonews.over-blog.com

news,sport,footbal,video,picture,comedy,ubbuyu,vichekesho,habari,taaria,breaking news

Madhara ya kutokulala usingizi wa kutosha

Kulala ni muhimu kwa mwili kama ilivyo kupumua. Unapokuwa umelala, ubongo wako hushughulika na afya yako ya mwili na akili ili ukuandaa kwa siku inayofuata.

kwa watoto na vijana, homoni ambazo huchochea ukuaji huachiliwsa na mwili wanapokuwa wamelala. Homoni hizi husaidia kujenga misuli, na pia kuzitengeneza seli na tishu zilizoharibika. Kulala ni muhimu sana kwa ukuaji wakati wa kubalehe.

Unapokosa usingizi, ubongo wako hautoweza kufanya kazi kwa ufanisi, jambo ambalo litaathiri uwezo wako wa utendaji kazi pamoja na hisia zako. Kama hali ya kukosa usingizi itaendelea kwa muda mrefu, basi inaweza kupunguza nguvu ya ulinzi wa mwili wako na kukuweka katika hatari ya kupata ugonjwa sugu.

Viashiria vya haraka kwa mtu asiyelala muda wa kutosha ni pamoja na kusinzia kila mara, kupiga miayo pamoja na kuwashwa. Kukosa usingizi kwa muda mrefu inaweza kuathiri usawa wa mwili, uratibu na uwezo wa kufanya maamuzi. Unakuwa na hatari ya kupata usingizi wakati wa mchana, hata kama utapambana na hali hiyo. Vichochezi kama kafeini na kahawa haviwezi kukuepusha dhidi ya hali ya mwili wako kutokuhitaji kulala.

Mwili unapokosa muda mzuri wa kulala, madhara ya pombe huongezeka maradufu na kukuweka katika hatari ya kupata ajali.

Kwa mujibu wa ‘Havard Medical School’ utafiti umeonyesha kuwa kulala kwa muda wa chini ya saa tano kwa siku huongeza hatari ya mtu kufa kwa asilimia 15. Kukosa usingizi ni hatari kwa afya ya mwili na akili na huweza kupunguza kiwango chako cha kuishi.

Mfumo mkuu wa neva

Unapolala unaupa ubongo wako muda mzuri wa kupumzika na kuifanya kaze yake kwa utulivu. Vilevile ubongo hutengeneza protini ambayo husaidia kuzihuisha seli zilizoharibika. Kwa watoto na vijana wanaobalehe, wakati wa kulala ndio wakati muhimu wa ubongo kufanya mabadiliko katika mwili na ukuaji. Unapokosa usingizi wa kutosha ina maana kuwa ubongo wako haupati muda mzuri wa kujituliza, hivyo utaathiri uwezo wako wa kujifunza mambo mapya na kuhifadhi kumbukumbu.

Mfumo wa upumuaji

Unapokosa usingizi wa kutosha, ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa hupungua, hivyo kujiweka katika hatari ya kupata madhara katika mfumo mzima wa upumuaji. Hii ni kwa sababu mwili hushindwa kupambana vyema na maradhi yanayoathiri mfumo huu kama vile mafua na vikohozi. Kama una ugonjwa wa mapafu, basi kutokulala kwa muda wa kutosha huufanya ugonjwa huo kuwa na madhara zaidi.

Mfumo wa mmeng’enyo

Kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na Havard Medical School, ulibaini kuwa kuna muunganiko kati ya kukosa usingizi na kuongezeka kwa uzito wa mwili. Pamoja na kula sana pasipo kufanya mazoezi, ukosefu wa usingizi humuweka mtu katika hatari ya kupata utapia mlo pamoja na ugonjwa wa kisukari.

Mfumo wa Kinga ya mwili

Unapokuwa umelala, kinga yako ya mwili hutengeneza seli za kupambana na bakteria, virusi, maradhi yanayouingia mwili pamoja na magonjwa mbalimbali. unapokosa uusingizi wa kutosha ina maana kuwa kinga yako ya mwili haijapata muda wa kujenbga ulinzi imara kwa ajili ya mwili wako. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ‘Mayo Clinic’ umeonyesha kuwa mtu asipopata usingizi wa kutosha anakuwa katika hatari kubwa ya mwili wake kushindwa kupambana na bakteria hatari wanaoingia. Vilevile inaweza kufanya mwili uchukue muda mrefu sana kupambana na magonjwa yanayokusumbua., hali inayoweza kukusababishia kuwa na magonjwa sugu.

Mfumo wa mishipa

Unapolala mwili wako huwa na uwezo wa kutibu na kujenga mishipa ya damu na moyo. Kukosa usingizi kwa muda mrefu huongeza hatari ya kuwa na matatizo sugu ya kiafya kama vile shinikizo kubwa la damu, ugonjwa wa moyo na kiharusi. Kulingana na utafiti wa ‘Havard medical School’ watu wenye shinikizo la damu wasipolala kwa muda wa kutosha kwa usiku mmoja tu, inatosha kupandisha shinikizo la damu kwa siku nzima inayofuata.

Kulala ni muhimu kwa mwili kama ilivyo kupumua. Unapokuwa umelala, ubongo wako hushughulika na afya yako ya mwili na akili ili ukuandaa kwa siku inayofuata. kwa watoto na vijana, homoni ambazo huchochea ukuaji huachiliwsa na mwili wanapokuwa wamelala. Homoni hizi husaidia kujenga misuli, na pia kuzitengeneza seli na tishu zilizoharibika. Kulala ni muhimu sana kwa ukuaji wakati wa kubalehe. Unapokosa usingizi, ubongo wako hautoweza kufanya kazi kwa ufanisi, jambo ambalo litaathiri uwezo wako wa utendaji kazi pamoja na hisia zako. Kama hali ya kukosa usingizi itaendelea kwa muda mrefu, basi inaweza kupunguza nguvu ya ulinzi wa mwili wako na kukuweka katika hatari ya kupata ugonjwa sugu. Viashiria vya haraka kwa mtu asiyelala muda wa kutosha ni pamoja na kusinzia kila mara, kupiga miayo pamoja na kuwashwa. Kukosa usingizi kwa muda mrefu inaweza kuathiri usawa wa mwili, uratibu na uwezo wa kufanya maamuzi. Unakuwa na hatari ya kupata usingizi wakati wa mchana, hata kama utapambana na hali hiyo. Vichochezi kama kafeini na kahawa haviwezi kukuepusha dhidi ya hali ya mwili wako kutokuhitaji kulala. Mwili unapokosa muda mzuri wa kulala, madhara ya pombe huongezeka maradufu na kukuweka katika hatari ya kupata ajali. Kwa mujibu wa ‘Havard Medical School’ utafiti umeonyesha kuwa kulala kwa muda wa chini ya saa tano kwa siku huongeza hatari ya mtu kufa kwa asilimia 15. Kukosa usingizi ni hatari kwa afya ya mwili na akili na huweza kupunguza kiwango chako cha kuishi. Mfumo mkuu wa neva Unapolala unaupa ubongo wako muda mzuri wa kupumzika na kuifanya kaze yake kwa utulivu. Vilevile ubongo hutengeneza protini ambayo husaidia kuzihuisha seli zilizoharibika. Kwa watoto na vijana wanaobalehe, wakati wa kulala ndio wakati muhimu wa ubongo kufanya mabadiliko katika mwili na ukuaji. Unapokosa usingizi wa kutosha ina maana kuwa ubongo wako haupati muda mzuri wa kujituliza, hivyo utaathiri uwezo wako wa kujifunza mambo mapya na kuhifadhi kumbukumbu. Mfumo wa upumuaji Unapokosa usingizi wa kutosha, ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa hupungua, hivyo kujiweka katika hatari ya kupata madhara katika mfumo mzima wa upumuaji. Hii ni kwa sababu mwili hushindwa kupambana vyema na maradhi yanayoathiri mfumo huu kama vile mafua na vikohozi. Kama una ugonjwa wa mapafu, basi kutokulala kwa muda wa kutosha huufanya ugonjwa huo kuwa na madhara zaidi. Mfumo wa mmeng’enyo Kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na Havard Medical School, ulibaini kuwa kuna muunganiko kati ya kukosa usingizi na kuongezeka kwa uzito wa mwili. Pamoja na kula sana pasipo kufanya mazoezi, ukosefu wa usingizi humuweka mtu katika hatari ya kupata utapia mlo pamoja na ugonjwa wa kisukari. Mfumo wa Kinga ya mwili Unapokuwa umelala, kinga yako ya mwili hutengeneza seli za kupambana na bakteria, virusi, maradhi yanayouingia mwili pamoja na magonjwa mbalimbali. unapokosa uusingizi wa kutosha ina maana kuwa kinga yako ya mwili haijapata muda wa kujenbga ulinzi imara kwa ajili ya mwili wako. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ‘Mayo Clinic’ umeonyesha kuwa mtu asipopata usingizi wa kutosha anakuwa katika hatari kubwa ya mwili wake kushindwa kupambana na bakteria hatari wanaoingia. Vilevile inaweza kufanya mwili uchukue muda mrefu sana kupambana na magonjwa yanayokusumbua., hali inayoweza kukusababishia kuwa na magonjwa sugu. Mfumo wa mishipa Unapolala mwili wako huwa na uwezo wa kutibu na kujenga mishipa ya damu na moyo. Kukosa usingizi kwa muda mrefu huongeza hatari ya kuwa na matatizo sugu ya kiafya kama vile shinikizo kubwa la damu, ugonjwa wa moyo na kiharusi. Kulingana na utafiti wa ‘Havard medical School’ watu wenye shinikizo la damu wasipolala kwa muda wa kutosha kwa usiku mmoja tu, inatosha kupandisha shinikizo la damu kwa siku nzima inayofuata.

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post